Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa inashangaza sana kuona mpaka sasa watu waliohusika na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji hawakufikishwa mahakamani.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la kuwaapisha Makamishna wa juu wa jeshi la polisi pamoja na mawaziri wapya wawili akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria na Dkt. Agustine Mahiga pamoja na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi.

“Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa, Tulionyeshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa sawa”, amesema Rais Magufuli

Hata hivyo, Oktoba 2018, akiwa Jijini Dar es salaam mfanyabiashara Mohemed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana ambao walitajwa kuwa ni raia kutoka nje ya nchi lakini baadaye alipatikana maeneo ya Gymkhana Jijini Dar es salaam.

 

RC Dkt. Kebwe aagiza kukamatwa kwa waliovamia mashamba
AAR yatoa matibabu bure kwa washiriki Kili Marathon 2019