Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru.

Rais Dkt. Magufuli amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge katika Ikulu ya Chamwino.

Aidha, akiwa Mkoani humo, Rais Dkt. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni rasmi katika shughuli mbalimbali za kiserikali.

Hata hivyo, Sherehe za Uhuru zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri, Jumamosi tarehe 09 Desemba, 2017

 

Chadema wakosa Polisi wa kuwasindikiza mahakamani
TFF yamlilia Joel Nkaya Bendera