Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  John Pombe Magufuli amekiri kushangazwa na mambo Mungu anavyoitendea Tanzania katika kipindi hiki.

Rais Magufuli aliyasema hayo wakati akihutubia katika mapokezi ya ndege aina ya ‘Air Bus’ A220-300.

Amesema kuwa kwa baraka ambazo Mungu amekuwa akiipatia Tanzania ni wazi haitashikika na kwamba mambo yataendelea kunyooka sana.

“Nataka niwahakikishie kadiri tunavyoendelea Tanzania haitashikika tutakuwa juu mno. Tanzania tunaweza na tutaweza, Mambo yananyooka mno mpaka mimi namshangaa Mungu,Mungu anatupenda na yupo pamoja na sisi”,amesema JPM

Aidha, pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kwamba Air Bus ni dege ya kwanza katika nchi za Afrika kutua Tanzania, hakuna nchi yoyote kuanzia North au South ambayo ina ndege kama hiyo.

Hata hivyo, Rais amemuagiza mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL kumpelekea majina ya watendaji wa Serikali 100 ambao wanakatiwa tiketi na Serikali lakini hawasafiri.

Pinda asimulia jinsi wapinzani walivyokuwa wanamtaka JPM
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 24, 2018