Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendesha harambee na kuchangisha jumla ya shilingi milioni 60 ambazo watapewa wajumbe wa Chama Cha Walimu ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu wa Chama hicho CWT

Ameendesha harambee hiyo hii leo katika mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika mkoani Dodoma kwa lengo la kuwagawia wajumbe hela ya chakula.

Aidha, Rais Magufuli alianzisha zoezi hilo kwa kutoa milioni 10 na baadaye Rais kuanza kuwaita viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi za Serikali ili waweze kuchangia fedha za chakula ambapo kwa ujumla ziliweza kupatikana jumla ya shilingi milioni 60.

Rais Magufuli milioni 10

Waziri Mkuu  Milioni 10

Waziri wa Elimu, Ndalichako milioni 6

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama  milioni 6

Mama Magufuli Milioni 1

Mama Majaliwa  Milioni 1

Spika wa Bunge Job Ndugai Milioni 5

Katibu Mkuu Tamisemi Milioni 4

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi  Milioni 4

Mstahiki Meya wa Dodoma Milioni 1

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Milioni 1

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika Milioni 3

Mkuu wa Chuo cha Dodoma Milioni 4

Mkurugenzi wa usalama wa taifa Milioni 4

Hata hivyo, Rais Magufuli aliagiza kuwa milioni 50 wapewe wajumbe wa CWT huku milioni 10 zikienda kwa walimu wanafunzi wa UDOM ambao walishiriki katika Mkutano huo, na kuagiza fedha hizo zifike kabla ya wajumbe hao hawajamaliza Mkutano wao

Tundu Lissu: Tusipate hofu Chadema hatujaanza kusalitiwa leo
Wabunge wawekwa kikaangoni