Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Jaji Mstaafu, Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema kuwa uteuzi wa Jaji Lubuva umeanza leo Juni 18, 2018.

Jaji Mstaafu Lubuva anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Ngubullu.

Aidha, Jaji Mstaafu Lubuva alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) 2015

Trump aitishia China, watunishiana misuli
Askofu mbaroni kwa utapeli wa mamilioni ya waumini