Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa kwa kuhudhuria katika shughuli za uzinduzi wa maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, akisema kuwa kitendo hicho ni cha kiungwana.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Maktaba hiyo, ambapo amesema kuwa Tanzania ni nchi ya kila mmoja hivyo suala la ushirikiano katika maendeleo ni jambo la busara na la kuungwa mkono.

“Siku zote huwa nasema, mheshimiwa Lowassa umekomaa kisiasa, ndio maana unahudhuria katika shughuli za kimaendeleo, maendeleo hayana, chama, kabila, dini, wala rangi,”amesema Rais Magufuli

Hata hivyo, Rais Magufuli amemtaka Edward Lowassa kujaribu kuwafundisha siasa za kiungwana wanasiasa wa vyama vya upinzani hata kama wengine wako Magerezani.

Wanafunzi ‘walioibia mitihani’ wapandishwa kizimbani
Manchester United kuikabili Young Boys bila Victor Lindelof

Comments

comments