Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemjulia hali Mama yake mzazi, Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam tangu miezi mitatu iliyopita baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (Heart Stroke).

Aidha, Rais Magufuli ameongoza maombi ya kumuombea Mama yake pamoja na watu wote wanaokabiliwa na maradhi na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2019.

Vilevile amewashukuru Madaktari na Wauguzi wanaomhudumia Mama yake na wagonjwa wengine nchini na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu heri na fanaka katika majukumu yao ya kunusuru maisha ya watu.

Kangi Lugola atangaza akaunti mpya za kijamii
Hasunga aagiza wakulima wasajiliwe

Comments

comments