Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Meja Jenerali, Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Aidha, Pamoja na uteuzi huo, Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali, James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Pia Rais Dkt. Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigadia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao.

1.Brig Jen. J.G. Kingu

2.Brig Jen. M.S. Busungu

3.Brig Jen. R.R. Mrangira

4.Brig Jen. B.K. Masanja

5.Brig Jen. G.T. Msongole

6.Brig Jen. A. F Kapinga

7.Brig Jen. K.P Njelekela

8.Brig Jen .A. S Bahati

9. Brig Jen. M.F Mkingule

10.Brig Jen .S.S Makona

 

Kyle Edmund ajitoa Argentina Open
Serena Williams arejea rasmi uwanjani