Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambaye jumamosi ya Machi 30, 2019 alifanya harambee kupitia kampeni yake ya ‘Tokomeza Zero’ iliyolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga shule ya bweni ya wasichana kuwasaidia kielimu iliyohudhuriwa na watu mbalimbali maarufu ikiongozwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Katika Harambee hiyo Mhe.Mwegelo alifanikiwa kukusanya milioni 915 kati ya sh.Bilioni 1.3 ambapo hadi kufikia jana tayari shilingi milioni 80 zilikuwa zimekwisha kusanywa na kuwekwa banki.

Jana Jokate alizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa mbali na michango hiyo iliyokusanywa wapo wadau wengine waliojitolea kujenga mabweni ya wasichana mawili yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 kila mmoja na lengo ni kujengwa kwa mabweni sita, wadau wengine wamejitolea kutoa mbao za kuezeka mabweni zenye gharama ya shilingi mil.10, mifuko 1890 ya saruji, lakini pia kampeni hiyo imesaidia kutoa mafunzo kwa walimu 220 amabo wamefundishwa namna bora ya kutoa elimu inayoendana na karne ya 21.

Aidha alichukua nafasi hiyo kuwashukuru wananchi na wadau wa maendeleo waliojitokeza kuchangia kampeni hii ya kuwakomboa watoto wa kike kwa kuwawekea mazingira rahisi ya kupata elimu.

Jokate ameongezea kuwa sababu ya kufanya kampeni hizi ni kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kufika kidato cha sita ambapo katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2017 jumla ya wanafunzi 4880 walimaliza kidato cha nne lakini wanafunzi 66 tu ndio waliofanikiwa kufika kidato cha 6.

Mlipuko wa moto waitetemesha Korea kusini
Video: Adam Mchomvu amshauri Diamond ‘atulize wenge’, ampa taji Ali Kiba

Comments

comments