Jogoo mmoja nchini Ufaransa ambaye mmiliki wake amempatia jina la Maurice, ameburuzwa mahakamani na majirani kwa kuwakera majirani kwa kuwika kila alfajiri.

Jogoo huyo analaumiwa kwa kusababisha kalele na familia moja katika kisiwa cha Oléron huko Ufaransa.

Mmiliki wake, Corinne Fesseau, amemkingia kifua kwa kusema kuwa Jogoo Maurice anafanya kile ambacho majogoo wote wanafanya ambacho ni ‘Kuwikaa’.

Aidha, Jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama.

Walalamikaji, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, walijenga nyumba yao ya mapumziko katika kijiji cha Saint-Pierre-d’Oléron miaka 15 iliyopita, lakini baadaye wakaigeuza kuwa nyumba ya kuishi walipostaafu.

Sababu moja iliyowafanya kuchagua sehemu hiyo ni utulivu wake lakini tatizo kubwa limekuwa ni Jogoo Maurice, ambaye amekuwa kero kwao kwani amekuwa akiwapigia kelele kila alfajiri anapowika.

Walalamikaji hao walipowasilisha malalamiko yao kwa mmiliki wa Jogoo huyo, Fesseau ambaye ameishi Oléron kwa miaka 35, mabishano makali yalizuka mpaka mzozo kati yao ukagonga vichwa vya habari ulipofikishwa mahakamani.

Hata hivyo, Fesseau, na majirani zake wengine, walisema hakuna mjadala kuhusu swala hilo kwasababu ufugaji wa kuku ni sehemu ya maisha ya vijijini na kwamba hawaelewi kwa nini walalamikaji wanaomba Jogoo huyo azuiwe kuwika.

 

Putin awasili Rome na kufanya mazungumzo na Papa Francis
Video: Haiwezekani utekwe harafu upatikane karibu na kwa shangazi yako- Kamanda Mambosasa