Beki wa majogoo wa jiji “Liverpool” Joel Matip amesaini mkataba wa muda mrefu utakaomuwezesha kuwatumikia wabababe hao wa ligi ya England hadi mwaka 2024.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 28, ameshafunga mabao mawili katika michezo tisa aliyocheza msimu huu, na amekua kivutio kikubwa kwa meneja Jurgen Klopp aliemsajili mwaka 2016 akitokea Schalke 04 ya Ujerumani.

Msukumo mkubwa wa kusiani mkataba wa muda mrefu kwa beki huyo kutoka Cameroon, umetoka kwa meneja Klopp ambaye anahitaji huduma yake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Msimu uliopita Matip alifanya kazi kubwa katika michezo ya ligi na kusaidia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya, kwa kuifunga Spurs katika mchezo wa fainali.

“Nina hisia nzito za furaha moyoni mwangu, tukio la kusiani mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kuitumikia Liverpoo limenipa faraja,” Alisema Matip.

“Liverpool ni klabu kubwa, kila mchezaji anatamani kuwa hapa, kwangu ni bahati kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa wa Ulaya, ninaahidi nitapambana zaidi ya ilivyokua miaka mitatu iliyopita.”

Matip alikosa michezo miwili iliyopita ya ligi kuu ya England, kufuatia majeraha yaliyomsibu, na kesho anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kitakachosafiri hadi Old Trafford, kupambana na Manchester United.

Naibu waziri Aweso aagiza mkandarasi kusimamishwa kazi
Ajinyonga chumbani kwake kisa madeni ya vikoba