Timu ya JKT Tanzania imerejea Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu ujao baada ya ushindi wa mabao 5-1 ilioupata jana  dhidi ya African Lyon.

JKT Tanzania zamani wakifahamika kama JKT Ruvu walitumia vyema uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo uliopo Mbweni JKT hivyo kutinga rasmi kwenye ligi msimu wa 2018/19.

Aidha baada ya ushindi huo timu hiyo imefikisha alama 31 kwenye michezo 12 na kuendelea kuongoza Kundi A, ikifuatiwa na Friends Rangers yenye pointi 22 kwenye mechi 12

Katika Kundi hilo limebakiwa na mechi mbili tu hivyo kimahesabu JKT Tanzania tayari wametinga ligi kuu kwani hata wakipoteza mechi zao zote bado hakuna timu itakayowafikia.

Hata hivyo, timu za Friends Rangers yenye pointi 22 na African Lyon yenye pointi 21 zinapambana katika mechi mbili za mwisho kuwania nafasi moja ya kupanda ligi kuu iliyobaki katika kundi hilo.

Marekani kuzikabili Urusi na China
Rais airejea hukumu ya kunyongwa