Timu ya JKT Ruvu inayoshiriki ligi daraja la kwanza kundi A msimu huu, itajulikana kwa jina la JKT Tanzania Sports Club, na ndiyo timu iliyopitishwa kumililikiwa na jeshi la kujenga taifa na maskani yake yataendelea kuwa makao makuu ya jeshi hilo mlalakuwa kwa wakati huu, mababadiliko haya yamekuja baada baada ya kupata maelekezo toka bodi ya ligi kwa taasisi kumiliki timu moja, taratibu zote zimefuatwa katika kutekeleza agizo hili.

Uongozi wa JKT Ruvu unatoa shukrani za dhati kwa bodi ya ligi na TFF kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kupitia mamlaka/idara zake wakati wa mchakato mzima kuhusu swala hili mhimu kwa ustawi wa taifa letu kupitia mpira wa miguu,  mwenyekiti wa JKT Ruvu luteni kanali Hassan Mabena alikwisha tolea ufafanuzi wa kina kuhusu swala hili kupitia baadhi ya vyombo vya habari,

 

Historia ya timu

Timu ya JKT Tanzania SC, ilinzishwa mwaka 1970 katika kambi ya JKT Mgulani Dar es salaam, na ilijulikana kwa jina la JKT Kabambe, mwaka 1973 timu hiyo ilihamishiwa katika kikosi cha Ruvu JKT mkoani Pwani, na mwaka 1975, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa JKT Ruvu na mwaka 1999 timu ya JKT RUVU ilihamishiwa makao makuu ya jeshi la kujenga taifa mlalakuwa jijini Dar es salaam, Desemba 12, 2017,timu hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa  JKT Tanzania SC na taratibu za kupeleka taarifa za maandishi zilianza kutekelezwa na mafanikio mazuri yamepatikana kufuatia zoezi hili, uongozi wa JKT Ruvu unawataka wadau mbalimbali kuyapokea mabadiliko hayo ya kisheria kwa mikono miwili.

Ushiriki FDL

Timu ya JKT Tanzania SC kwa sasa inaendelea na kambi katika uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo -Mbweni JKT, chini ya kocha mkuu Bakari Shime, tayari kwa mchezo wake na timu ya Mvuvumwa FC utakaochezwa January 13 katika uwanja wa uhuru.

Mipango na malengo ya kocha mkuu Bakari Shime ni kuhakikisha timu inashinda katika michezo yote iliyobaki ili kutimiza malengo waliojiwekea, na wachezaji wote waliopo kambini wapo ari kubwa kuelekea mchezo huo

Azam FA Cup

Pamoja na ushiriki katika ligi daraja kwanza timu hii ina jukumu la kuweka ushindani mkubwa katika mashindano ya Azam FA Cup, ambapo timu imesonga mbele na imepangwa kucheza dhidi ya Polisi Dar katika hatua inayofuata, ndiyo maana kocha Bakari Shime ameiandaa timu yake kwa mashindano yote mawili.

Pamoja na kuwa na ushindani mkubwa Shime amekiri hiyo ni changamoto kubwa katika kuleta matokeo chanya kwa upande wa timu yake.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 6, 2018
Friends Rangers yapewa pointi za mezani