Ofisi ya Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, imesikitishwa na baadhi ya watu wanaotafsiri tofauti hotuba yake, Aliyotoa kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere.

Taarifa hiyo iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Oktoba 11, imeeleza masikitiko yake kuhusu upotoshaji huo wa hotuba aliyoitoa Oktoba 8, 2019, katika Kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mhe. Kikwete alizungumza juu ya namna ambavyo anamfahamu Hayati Mwalimu Julius Nyerere lakini hakumlinganisha na rais mwingine yeyote kama ambavyo watu wamekuwa wakipotosha.

Kwani kumekuwa na udanganyifu mkubwa ambao ulitafsiri hotuba ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amewasema marais wengine jambo ambalo amelikanushwa.

 

Kiongozi aburuzwa nyuma ya gari kwa kutotimiza ahadi za uchaguzi
Video: Ditram Nchimbi alizima simu alivyoitwa Stars na Ndayiragije, Kelvin John 'mazoezi magumu'