Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete jana ametoa mbinu mpya itakayokihakikishia chama hicho ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao umeonekana kuwa na ushindani mkali zaidi ya chaguzi zote zilizopita.

Akiongea jana katika uzinduzi wa kampeni za urais za chama hicho Zanzibar ulifanyika katika uwanja wa Kibanda Maiti, Dk Kikwete aliwaeleza wafuasi wa chama hicho kuwa uchaguzi wa mwaka huu sio wa kushinda hivihivi bali inapaswa kufanya kampeni kwa juhudi kubwa.

Aliitaja mbinu ya mpira wa miguu inayotumika wakati ambapo kuna ushindani mkali ya ‘Man To Man’ yaani mtu na mtu, kuwa ndiyo inayopaswa kutumiwa na chama hicho katika uchaguzi wa mwaka huu.

“Ingekuwa mpira wa miguu tungesema ni ‘man to man’, lazima umjue mtu wako na umkabe kisawasawa,” alisema.

“Uchaguzi huu mwaka huu ni kiambo kwa kiambo, nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda, shuka kwa shuka,” aliongeza.

znz5

Hata hivyo, alisisitiza kuwa ana imani CCM itashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu licha ya ushindani uliopo.

Kwa upande wake mgombea urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, alisema kuwa ana imani atashinda katika uchgauzihuu kwa kuwa ameridhshwa na utekelezaji wa ilani ya CCM iliyoiletea Zanzibar maendeleo makubwa.

Ndoa Ya Spurs Na Adebayor Yavunjika Rasmi
Amani Karume Achukizwa Na Lugha Za Matusi Kwenye Kampeni Ya CCM