Mara mtu apatapo mafanikio mambo mengi hutokea au huabdilika moja ya mambo amabyo hutokea ni mabadiliko kwa watu wano mzunguka mtu huyo, wengine humpenda wengine humchukia au hata kumuonea wivu.

Kwakuwa wivu huwa athiri wale walionao pekee ni vyema na wewe ukafahamu tabia za watu wenye wivu ili uwaepuke wasije wakakuathiri kwa kukurudisha katika hatua za maendeleo.

Hawastaajabishwi na mafanikio ya mwingine  hata wasikie jambo zuri au kubwa  kiasi gani la mtu mwingine wao huliona kama la kawaida, unaweza kusikia wakisema kauli kama ”mbona haya mambo ya kawaida”,”mbona wapo wengi waliofika hapo”,” mambo ya kupita hayo”,”cha muhimu uzima bwana” watu kama hawa ni wa kuwaepuka maishani kwani wivu umewatawala.

Wanapenda kuiga na kushindana kwa kawaida watu hawa ni wale wasiokua na malengo wala maono yoyote, watu hawa huangalia wanayoyafanya au wanavyoishi watu wengine na kuiga watu wa aina hii ni wenye wivu na watakunyonya nguvu ikiwa utashiriki kwenye mashindano yao.

Hupenda kuleta taarifa mbaya kuna watu ambao kila mara wao ni kuleta taarifa mbaya hasa juu ya jitihada zako za kimaendeleo au dhidi ya malengo yako, unaweza kusikia watu hawa wakisema ”aaah yule jamaa mwenye biasha kama yako amefilisika”inavyoonekana biasha kama hiyo yako huko tunakoelekea haitakuwa na dili, tabia ni ya watu wenye wivu wakitaka tu kukurudisha nyuma ili ukate tamaa.

Hufurahia wengine wanaposhidwa mtu anayefurahia kushidwa ua kuanguka kwa mwingine basi ujue kiwango chake cha wivu ni kikubwa sana, kwa kuwa watu wenye wivu huwa hawapendi kuona meli ya mtu mwingine baharini.

Hupenda kujikweza na kujionesha watu wenye wivu hukosa unyenyekevu wao hupenda kuonyesha kuwa wapo juu ya kila mtu na hupenda kutambulika kwa kila mtu, watu hawa pia hutoa ushauri mbaya hawapendi watu wengune wafanikiwe basi wao huwapa wengine ushauri ambao utawakwamisha.

Hukupa sifa za uongo kuna msemo usemao ”sifa zinaua” watu wenye wivu hujifanya wanakukubali na hivyo kukupa sifa za uwongo ili zikuangamize, ili kulinda malengo yako hakikisha huendeshi maisha yako kwa kutegemea sifa za watu wengine.

Video: TCRA - Tunazima laini zisizosajiliwa, Wengi waachwa
Tumia hivi ndizi kwa urembo wa uso