Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga yaingia Mjini Songea na kuleta neema kwa wafanya biashara wa jezi mbali mbali za wachezaji wao huku jezi ya kiungo kutoka Congo Tshishimbi Kabamba ‘Papii Kabamba’ ikiongoza kwa mauzo.

Yanga leo inacheza na Majimaji mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Majimaji ikiwa imetoka kuifunga Njombe Mji bao 1-0 wikiendi iliyopita.

Katika mitaa mbalimbali ya Songea, wafanyabiashara ndogondogo wanaonekana wakiwa na jezi zinazotumiwa na Yanga zenye jina na namba ya Tshishimbi na zile za Chirwa na wachezaji wengine wakiziuza kwa mashabiki.

Jezi hizo zinazouzwa nje ya utaratibu wa klabu, huuzwa kwa kati ya Sh 7000 hadi Sh 25,000 na mashabiki wamekuwa wakizichangamkia kuzinunua.

Juzi jezi ya Tshishimbi ilikuwa ikinunuliwa kwa wingi lakini jana Ijumaa ile ya Chirwa raia wa Zambia nayo ilinunuliwa kwa wingi.

Morata aeleza sababu za kuitosa Man Utd
Bavicha walivimbia Jeshi la Polisi

Comments

comments