Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Mara, limetoa taarifa rasmi juu ya kuokotwa kwa mwili wa mfanya biashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ambaye alitoweka na mwili wake kuokotwa mtoni hapo jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamedi amesema kuwa hapo jana walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuokotwa kwa kiroba chenye mwili ndani, na walipokifungua na kuita watu kutambua ndipo alipojulikana kuwa ni mwili wa mfanya biashara huyo anayeishi Jijini Mwanza.

“Wananchi waliona kiroba kimefungwa kinaelea, kikavutwa wakajulishwa polisi kufungua ndani wakakuta mwili wa marehemu, kwa sababu tulikuwa na taarifa za utafutaji na mashaka juu ya kutoweka kwake, tukajulisha ndugu hao na wakatambua mwili wa marehemu”, amesema Kamanda Mohamed

Aidha, Kamanda Mohamed amesema kuwa marehemu alitoweka kuanzia tarehe 27 mwezi wa pili ambapo aliondoka mkoani mwanza, na ndugu zake walisema kuwa aliaga anaenda Simiyu kwa shughuli zake za kibiashara na kuna mtu anamdai na akapotea tangu siku hiyo na gari yake aliyotoka nayo Mwanza kukutwa imechomwa mtoto maeneo ya Serengeti mnamo tarehe 8 hadi kuteketea kabisa.

Hata hivyo, kwa sasa mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa ajili ya uchunguzi na baadaye utatolewa kwenda kuzikwa, ambapo mpaka sasa watu wanne wanashikiliwa kufuatia tukio hilo.

Mhudumu aanguka kutoka kwenye ndege Uganda
Masoud Djuma: Tutapambana hadi tone la mwisho