Jeshi la polisi mkoani Mtwara limewaonya wanasiasa wanaofanya mikusanyiko isiyo halali kwa madai ya kulinda kura katika uchaguzi mdogo unaotegemewa kufanyika kesho Jumapili huku lilikitoa wito kwa wananchi kujitokeza kutekeleza haki yao ya kidemokrasia na kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Angalizo hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya ambapo amesema kuwa jeshi hilo limejipanga na lina askari wa kutosha kutuliza ghasia katika Uchaguzi wa madiwani na ubunge kesho.

“Tutatakuwa na askari wengi sana katika vituo vyote vinavyotarajiwa kupigwa kura, kwa hiyo mtu yeyote asijipe jukumu hilo, hivyo vyama vinavyojipanga kutekeleza jukumu la polisi hatujaomba msaada sisi,”amesema Kamanda Mkondya

Hata hivyo, kwa upande Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeridhia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu na madiwani Tanzania bara baada ya kuridhika na uendeshaji wa kampeni kwa vyama mbalimbali ambazo zinamalizika rasmi hii leo.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 12, 2018
Zitto: Wajibu wangu kuiharibu CCM, mtasubiri sana