Jeshi la Polisi limesema kuwa limepokea agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangalla la kuwakamata watu wanne ndani ya siku saba kwa madai ya kwamba wanashiriki katika mtandao wa ujangiri, lakini hawafanyi kazi kwa shinikizo.

Hayo yamesemwa hii leo na msemaji wa jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa, ambapo amesema kuwa Jeshi hilo linafanyakazi kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za jeshi hilo na si kwa shinikizo.

Amesema kuwa jukumu lao ni kukamata wanapopata shitaka la kuwepo kitu kisicho cha kawaida, kuchunguza na kupeleka kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa ajili ya kukamilisha hatua nyingine.

“Kazi yetu ni kukamata, kuchunguza na kupeleka kwa DPP kwa ajili ya kuchukua hatua nyingine, hivyo hatufanyi kazi kwa shinikizo na matamko ya bungeni,”amesema Mwakalukwa

Hata hivyo, ameongeza kuwa alichokisema Dkt. Kigwangalla amekisoma kwenye vyombo vya habari, hivyo hawafanyi kazi kwa kuangalia vyombo vya habari vimeandika nini.

 

Ruby: Niliamua kuomba msamaha, Ruge Mutahaba ni kama baba yangu
Video: Wastara akikabidhiwa milioni 15