Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za mauaji, wizi pamoja na kukutwa na noti bandia ambazo wamekuwa wakizitumia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa 10 kati ya hao wanaoshikiliwa wanatuhumiwa kwa kosa la mauaji, watatu kwa tuhuma za wizi na mmoja kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia.

Aidha, kwa mujibu wa Kamanda Mtafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako uliofanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa huo na kubaini watuhumiwa hao wakiwemo 10 waliotekeleza mauaji kwa imani za kishirikina.

 

Putin aipa kisogo mahakama ya kimataifa, kumneemesha Bashir
Gari lenye mabomu laua 14 karibu na hoteli