Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewashinda wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika hivi karibuni na kufanikiwa kuwaokoa watu 178 waliokuwa wakishikiliwa na kundi hilo.

Msemaji wa jeshi hilo aliiambia BBC kuwa watu hao ni pamoja na watoto, wazee na wanawake waliokuwa wakishiliwa na wanamgambo hao kwa muda mrefu katika jimbo la Borno.

Seneta anaewakilisha Borno alisifia hatua zinazochukuliwa na rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari na jinsi alivyojitoa kukabiliana na wanamgambo hao.

“Hivi karibuni mkuu wa majeshi aliteuliwa na akaingia moja kwa moja kazini, alikuwa na kikosi cha jeshi mstari wa mbele. Hiyo iliongeza morali na kuwafanya wanajeshi kujitoa zaidi kupambana dhidi ya wanamgambo hao,” alisema gavana huyo.

Katika hatua nyingine, kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau amekosekana kwenye vipande vya video vilivyotolewa na kundi hilo hivi karibuni. Hali hiyo imezua maswali mengi kuwa huenda amefariki dunia au amejeruhiwa vibaya.

Mara ya mwisho, Shekau alisikika kwenye kipande cha sauti mwezi Machi mwaka huu na tayari kundi hilo limeshatoa vipande viwili vya video.

Wanamgambo wa Boko Haram bado wanawashikilia wasichana wa shule zaidi ya 200 waliowateka katika maeneo mbalimbali nchini humo. Inadaiwa kuwa tayari wameshaanza kuwafundisha ugaidi na kuwatumia kujitoa mhanga katika baadhi ya matukio.

Kulitokomeza kundi la Boko Haram ni kipaumbele cha kwanza cha rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari.

 

Rais Nkurunzinza Atoa Onyo Baada Ya Mauaji Ya Jenerali Wa Jeshi Lake
Ferguson Amshukuru Rooney