Mwanamke mmoja raia wa Uingereza anakabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela Mjini Dubai kwa kutoa lugha ya matusi  kwa mke wa mtalaka wake katika Mtandao wa kijamii wa facebook.

Laleh Shahravesh mwenye umri wa miaka 55, alikamatwa mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Dubai kuhudhuria mazishi ya mume wake wa zamani.

Hata hivyo ameshitakiwa kutokana na maneno aliyoyachapisha katika mtandao huo baada ya mtalaka wake kuoa tena mwaka 2016.

Bi. Shahravesh alikua kwenye ndoa kwa miaka 18 na aliwahi kuishi Dubai kwa miezi 18,ambapo alirejea Uingereza na kumuacha mtalaka wake Dubai na kuoa mke mwingine  kwa mujibu wa mamlaka mji hapo.

Sharavesh alifahamu kuhusu hatua ya mtalaka wake kuoa tena baada ya kuona picha ya wanandoa hao katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Aliandika maneno ya matusi kwa lugha ya Kiajemi, na kuongeza kuwa mtalaka wake ni ”mjinga na kumuita farasi mke wake mpya”.

Sheria ya mtandao katika falme za kiarabu mtu anaweza kufungwa jela au kutozwa faini kwa kutoa kauli za chuki mtandaoni.

Aidha Maafisa mjini Dubai wanasema kuwa Bi Shahravesh huenda akafungwa jela miaka miwili au kutozwa faini ya pauni 50,000, licha ya kuchapisha maneno hayo akiwa nchini UIngereza.

Nae afisa mtendaji mkuu wa shirika la Detained in Dubai, Radha Stirling, ameiambia BBC kuwa ofisi ya uhamiaji ilimuomba mlalamikaji kuondoa madai hayo, lakini amekataa kufanya hivyo.

Bi Stirling amesema kuwa mteja wake ameachiliwa kwa dhamana lakini pasipoti yake imechukuliwa na kwamba kwa sasa anaishi katika hoteli.

Ameongeza kuwa watu huenda hawana ufahamu kuhusu sheria kali za uhalifu wa mtandaoni katika Falme za Kiarabu na idara ya uhamaji ya nchi hiyo haijatoa onyo kwa watalii.

 

Video: Mke wangu nampiga kwa tishu - Foby
Nguo za ndani za mtumba zapigwa msako kuondolewa