Ndoa ya bilionea, Jeff Bezos na MacKenzie imevunjwa rasmi ijumaa wiki iliyopita, Jaji wa mahakama ya kitongoji cha King mjini Washington alisaini talaka rasmi ya kuwatenganisha wawili hao ambao walidumu kwa miaka 25.

Wawili hao wamegawana mali walizochuma ikiwemo utajiri wa pesa ambapo Bi MacKenzie ameondoka na asilimia nne ya mali hizo ambayo thamani yake ni $38.3 bilioni sawa na Trilioni 88 za kitanzania.

Jeff Bezos mwenye umri wa miaka 54, alitajwa na Bloomberg Billionaire Index kuwa mtu tajiri zaidi duniani, akiwa na utajiri wa $137 bilioni, ambao unazidi utajiri wa Bill Gates kwa $45bilioni.

Aliyekuwa mke wa bilionea huyo MacKenzie, mwenye umaarufu wa uandishi wa vitabu na mfanyabiashara, baadhi ya vitabu maarufu alivyowahi kuviandika ni pamoja na The Testing of Luther Albright cha mwaka 2005 na Traps cha mwaka 2013.

Hata hivyo Jeff ameondoka na  asilimia 12, $114.8 bilioni sawa na Trilioni 261.9 za kitanzania na kumbakiza namba 1 kwenye orodha ya matajiri Duniani.

LIVE CHATO : Rais John Pombe Magufuli akizindua hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi
Ujerumani yapuuza ombi la Marekani

Comments

comments