Japan imepata pigo la kuporomoka kwa idadi ya watu na watoto waliozaliwa mwaka huu, kwa mujibu wa takwimu za Serikali ya nchi hiyo.

Takwimu hizo za Serikali zimeonesha kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa imepungua kwa kasi mwaka huu hadi 921,000, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi kushuhudiwa tangu walipoanza kuweka kumbukumbu hizo mwaka 1899, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi wa Jamii.

Idadi ya watoto wanaozaliwa inakadiriwa kushuka kwa zaidi ya 25,000 kutoka mwaka 2017, na idadi ya wanaozaliwa inabaki kuwa chini ya milioni moja kwa miaka mitatu mfululizo.

Aidha, kiwango cha vifo pia kimezua taharuki, kikifikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa cha watu milioni 1.369, huku idadi ya watu ikipungua kwa 448,000, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea cha kupungua kwa idadi ya watu.

Japan inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya wazee, ikirekodiwa kuwa zaidi ya 20% ya watu wake ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 65. Nchi hiyo ina idadi ya watu milioni 124 lakini kutokana na hali iliyopo inatarajiwa kuwa hadi kufikia mwaka 2065 inatarajiwa kushuka kwa takribani watu milioni 88.

Kolasinac: Ozil amewanyamazisha, tuko nyuma yake
Pinda asimulia jinsi wapinzani walivyokuwa wanamtaka JPM