Japan, Marekani na Korea ya Kusini zimeungana kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi wiki hii kwa lengo la kujihami na Korea Kaskazini.

Hatua hiyo, imekuja mara baada ya viongozi wa Korea Kaskazini kufyatua kombora la nyuklia lenye uwezo wa kushambulia toka bara moja hadi jengine.

Aidha, mazoezi hayo pamoja kati ya Japan, Marekani na Korea ya Kusini yanafanyika karibu na pwani ya Japan eneo ambalo limependekezwa na nchi hizo.

Taarifa zilizotolewa na Marekani zinasema kuwa nchi hiyo imedhamiria kuendeleza ushirikiano wake pamoja na nchi zote hizo mbili mpaka pale Korea Kaskazini itakaporejea katika meza ya mazungumzo kuhusu namna ya kuachana na silaha za nyuklia.

Hata hivyo, Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ameonya dhidi ya hatari inayoweza kusababishwa na uamuzi mbaya katika ugonvi huo na Korea ya kaskazini.

 

 

Gambo amtabiria makubwa Lema
JPM ataka bodi ya wadhamini UVCCM ivunjwe