Mtandao wa Jamii Forums umekanusha madai yanayosema wameanzisha Jamii Forums mpya nchini Kenya na kutoa tahadhari kwa wateja wake juu ya uzushi wa taarifa hiyo na kuomba wapuuzie taarifa hiyo.

Hivyo kupitia ukurasa wake wa Twitter umetoa tahadhari kwa wateja kujiepeusha na taarifa zinazosambaa katika mitandao mbalimbali na kuwataka wateja kuepuka kuweka taarifa zao walizotumia katika jukwaa la Jamii Formus hapo awali.

Uzushi huo ni kufuatia agizo lililotolewa na Mamlaka ya kudhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanza kutumia sheria ya maudhui ya mtandao inayowataka watoa maudhui mtandaoni kuwa na leseni ya utoaji wa huduma hiyo hali iliyopelekea Jamii Forums kutii agizo hilo bila shuruti kwa kusitisha huduma hiyo.

Mkurugenzi na mwanzilishi wa jukwaa la Jamii Forums Maxence Melo nae ameongezea kuwa Jamii Forums haijahamishiwa Kenya kama inavyodaiwa.

”Hatujahamisha Jamii Forums Kenya, hao wanaoonesha jukwaa hilo inawezekana wameona Tanzania imezuia sauti za watu kwa hiyo wamezichukua wao. Kama sauti zetu zinazuiwa wengine wanachukua wanaendelea” Amesema Maxence Mello.

Aidha Melo amesema tangu walipoamua kusitisha huduma zao wamefanya jitihada za kuzungumza na TCRA bila mafanikio ila wamesisitiza kuendelea kuwatafuta ili kupata suluhisho.

 

 

Video: Jeshi la polisi lathibitisha usalama na ulinzi sikukuu ya Eid El-Fitri
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Japan