Maombi ya mtuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi James Rugemalira, ya kutaka aachiwe huru yamepingwa na upande wa jamhuri kwa madai kuwa yamepelekwa wakati ambao sio muafaka na mahakama haina mamalaka ya kutoa amri hiyo.

Jamhuri iliwasilisha hoja hizo jana katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu mbele ya hakimu mkazi mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.

Wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon, alidai kwamba kesi ilienda kwa ajili ya kutajwa na tayari wameshafaili majibu ya pingamizi la awali lililowasilishwa na washtakiwa.

Amedai kuwa katika majibu yao wameiomba mahakama itupilie mbali maombi hayo kwa sababu yamewasilishwa wakati ambao sio muafaka na mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri kama ambavyo mshtakiwa anaomba.

Ikumbukwe kuwa katika barua za Rugemalira kwa mahakama amedai kwamba amemtaka Gavana wa Benki kuu (BOT) atoe orodha ya waliopewa fedha kutoaka akaunti ya Tegeta Escrow ili yeye asafishike kwa sababu hajalipwa hata senti moja kutoka katika akaunti hiyo.

Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni mwenyekiti mtendaji wa PAP wanadaiwa kutenda makosa ya uhujumu uchumi katika nchi za Afrika kusini, Kenya na India kati ya Octoba 2011 na Machi 20114.

Serikali yavunja mkataba uliomchomoa Kangi Lugola
Magufuli: Ugonjwa huu unaua "tukidharau tutakwisha"

Comments

comments