Msemaji wa klabu ya soka ya Simba, Haji Manara amekiri kupata kitete wakati anaongea kwenye Podium ya Ikulu, wakati Rais Magufuli alipowaalika wachezaji wa Taifa Stars kwaajili ya chakula cha mchana, ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza kwa ushindi dhidi ya Uganda.

Manara akiwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya (Saidia Taifa Stars Ishinde), alipata nafasi ya kuongea ambapo mwenyewe ameeleza kwa mara ya kwanza amepata kitete.

”Jamani Ikulu muisikie hivyo hivyo, leo kwa mara ya kwanza wakati naongea pale kwenye ‘Podium’ ya Ikulu kitete kilinijaa,”amesema Manara.

Aidha, Manara ambaye ni hodari wa maneno hususani akiwa kwenye eneo lake la usemaji wa Simba, ameeleza kuwa ushindi wa Taifa Stars umepeleka furaha kwa viongozi wakuu wa nchi Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa pamoja na heshima kwa Watanzania wapenda soka.

Hata hivyo, Rais Magufuli leo Machi 25, 2019 amekutana na wachezaji wa timu ya taifa, pamoja na bondia Hassan Mwakinyo ambaye Jumamosi usiku alipigana pambano lisilo la ubingwa na Muargentina Sergio Eduardo Gonzalez na kumchakaza.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 26, 2019
Flaviana Matata atokea kwenye tangazo la Rihanna

Comments

comments