Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wakuu wa mikoa kubuni mikakati ya kuondoa tatizo la ombaomba mijini.

Waziri Jafo ameyasema hayo alipokuwa akizindua Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam ambao umelenga kuvutia watalii mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya jiji hilo.

Katika uzinduzi huo, Jafo amesema ombaomba hao wamekuwa wakikaa barabarani hali ambayo haileti sura nzuri kwa nchi na kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii nchini.

Waziri Jafo amesema changamoto ya watoto wa mitaani na tatizo kubwa la ombaomba ni vyema wakuu hao wakabuni mbinu mbalimbali zikiwemo za kuwawekea maeneo maalum ya kujihusisha na shughuli za ufugaji na kilimo cha bustani ili kuwaondoa mitaani.

“Tukifanya hivi tutakuwa tumefanikiwa kuondokana na kitendo cha wao kukaa barabarani kwa kuwa hakileti sura nzuri kwa nchi yetu kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii hapa nchini,”amesema Jafo.

Polepole: Zitto Kabwe ajiandae kutafuta kazi ya kufanya
Kwa nini shule za Serikali zinaongoza kwa ufaulu mbovu mitihani ya taifa?