Jacqueline Ntuyabaliwe ambaye ni mke wa marehemu Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, leo kwenye siku ya kuzaliwa mume wake amefunguka kwa mara ya kwanza tangu kitokee kifo cha Mengi.

Kupitia mtandao kwenye ukurasa wake wa Twitter Jacqueline ameandika maneno mazito ambayo yatagusa hisia za watu wengi na pengine kutonesha donda la kumpoteza tajiri huyo mkubwa nchini aliyekuwa kimbilio la wengi wenye uhitaji.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika.

”Today we would have been celebrating you,if I close my eyes I can see how you would have smiled when we sing happy birthday to you. There are no words to describe how much I and the kids miss you,waking up each day without you. Happy birthday my true love,forever in our hearts”.

Akimaanisha; Leo tungekuwa tunasherekea siku yako ya kuzaliwa, Nikifumba macho yangu nakuona jinsi ambavyo ungekuwa unatabasamu wakati tukikuimbia wimbo wa kukutakia heri katika siku yako ya kuzaliwa. Hakuna neno litakaloweza kuelezea jinsi gani mimi na watu tunakukumbukua, kila tuamkapo asubuhi bila uwepo wako. Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu wa kweli, daima utaishi mioyoni mwetu”.

Katika maisha hakuna kitu kigumu kama kumpoteza mtu aliyekuwa karibu na maisha yako, itachukua muda mrefu kukubali hali lakini pia kuizoea, Mrs Mengi bado anauguliwa na machungu ya kuondokewa na mume wake ambaye hajaishi naye kwa muda mrefu tangu walipo kula kiapo cha kifo kuwatenganisha yaani ndoa.

Aidha, Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 akiwa katika falme za kiarabu huko Dubai ambako alienda kwa mapumziko na gafla kushikwa na ugonjwa ambao ulimchukua maisha yake.

Mungu aendelee kuipumzisha roho yake mahali pema peponi.

Nyalandu ashikiliwa tena na polisi, atoka kwa dhamana
Video: Mwanamke mwenye misuli zaidi duniani

Comments

comments