Klabu ya Aston Villa imeikataa ofa ya Pauni milioni 25 iliyotumwa na uongozi wa Tottenham, kwa lengo la kumsajili kiungo kutoka nchini England Jack Grealish.

Aston Villa wameikataa ofa hiyo na kutangaza kuwa, mchezjai huyo mwenye umri wa miaka 23 hauzwi, na badala yake ataendelea kuwa na klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba uliopo.

Grealish, amekua katika mipango ya kutaka kuihama klabu hiyo ya Villa Park, kwa lengo la kucheza ligi kuu pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, lakini mpango huo hatoufanikisha baada ya ofa yake kukataliwa.

Hata hivyo tayari mchezaji huyo ameshaueleza uongozi wa Aston Villa, hatosaini mkataba mpya, ili kukidhi haja ya kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru pindi muda utakapowadia.

Image result for Jack Grealish not for saleMauricio Pochettino

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amewahi kukiri kuwa shabiki mkubwa wa Grealish, kufuatia kiwango cha soka lake anachokionyesha kila anapopata nafasi ya kuitumikia Aston Villa, na kama angefanikiwa kumpata katika kipindi hiki, angekua ametimiza lengo la kuwa karibu na mchezaji huyo.

Mpaka sasa Spurs hawajafanya usajili wa mchezaji yoyote, huku dirisha la usajili kwa England likitarajia kufungwa mishale ya saa kumi na moja jioni kwa saa za nchi hiyo

LIVE IKULU: Rais Magufuli na Rais Yoweri Museven wakizungumza Ikulu
Danny Rose kuhamia Ujerumani?

Comments

comments