Izzo Bizness ameeleza jinsi alivyotumia kupanda kwa Hamisa Mobeto hadi kupewa mchongo wa kutumbuiza Marekani, kama kilio cha kuwashtua wadau wa muziki kuwaona wasanii wengine.

Mkali huyo wa ‘Ridhiwani’, amefunguka kwenye The Playlist ya Times Fm baada ya kutakiwa kuelezea sababu za kusikika kwenye wimbo wake wa ‘Pepa’ aliomshirikisha Gosby akisema, “wakali wanasugulia, Bongo show za ng’ambo mpe Hamisa.”

Hamisa Mobeto amewahi kupewa nafasi ya kutumbuiza nchini Marekani akiwa na mwimbaji Christian Bella, baada ya kuachia wimbo wake ‘Madam Hero’.

Alisema aliamua kuuweka mstari huo kama mfano na kama namna ya kuwaamsha wadau kuwakumbusha kuhusu wasanii wengine wakali ambao wako kwenye muziki tena kwa muda mrefu.

“Ilikuwa ni mfano tu na kwa sababu ni mtu ambaye ameonekana. Kwa sababu ukitaja kwa waimbaji siamini kwamba Hamisa ameanza kuimba kipindi cha miaka kumi au 13 iliyopita… lakini amekuja na anaheshimu kazi yake anayofanya. Kafanya vizuri wamemuona wamemchukua wamempa shows,” alifunguka.

“Lakini ilikuwa work up call (uamsho) pia kwa wadau kwamba ‘huyu mmemuona kuna wapo pia wakali… unaweza kuwa umewachukulia poa na nini, lakini nao pia inabidi wakumbukwe,” aliongeza.

Izzo Bizness

Izzo amedai kuwa ingawa hana nia ya kuwalaumu wadau kwa changamoto za matamasha na ukuaji wa sanaa ya muziki ukilinganisha na kipindi cha nyuma, upigaji wa nyimbo za wasanii fulani tu kwenye redio kwa karibu wiki nzima mfululizo na kuwaacha wengi nyuma ni sehemu ya changamoto.

TID awatolea uvivu wasanii, ‘watoto wanakuwa mashangingi’
Zari azua hofu na drip sita kitandani, asema shetani muongo