Siku chache baada ya kifo cha ghafla cha Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Amadou Gon Coulibaly, Makamu wa Rais wa nchi hiyo Daniel Kablan Duncan amejiuzulu.

Imeelezwa kuwa, Makamu huyo anaachia nafasi kutokana na sababu binafsi na kwamba aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa mara ya kwanza mwezi Februari.

Kifo cha ghafla cha Coulibaly ambaye alikuwa chaguo la Rais Alassane Ouattara kurithi kiti cha Urais kimepelekea Chama tawala kuanza kutafuta upya Mgombea, mchakato ambao Wachambuzi wamesema unaweza kusababisha mvutano.

Kufuatia kifo cha Coulibaly aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo kwa muda mrefu, Chama tawala cha RHDP kimesema kinaweza kumuomba Rais kufikiria kuongeza muda.

Kocha Sven awasihi wachezaji Simba SC
Hai: Watuhumiwa dawa za kulevya, gongo watoroka mahabusu