Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imetoa onyo kwa kituo cha runinga cha ITV na Radio One kwa kurusha taarifa zisizo na ukweli kuhusu maandamano ya kuchukua fomu ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Taarifa hizo zilirushwa kama habari mpasuko (Breaking News) zikieleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano ya kumsindikiza mgombea huyo katika ofisi za Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi (NEC).

Jana, Vituo hivyo vilianza kuomba radhi katika taarifa zake za habari kama sehemu ya masharti ya waliyopewa na Mamlaka ya Mawasiliano, kuomba radhi kwa siku mbili.

Tamko la TCRA lilitolewa jana kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka hiyo, Bi. Magret Munyagi.

Irene Uwoya Apata Tiketi Ya Kuingia Bungeni, Sasa Ni Mheshimiwa
Lowassa Ashindwa Kuhudhuria Mazishi Ya Kisumo, Polisi Wakata Msafara