Iran imekanusha tuhuma za kuhusika na mashambulizi ya meli za mafuta katika Ghuba ya Oman, jambo ambalo inaliita kuwa ni la kushangaza.

Imesema kuwa jukumu lake ni kusimamia ulinzi wa Mlango wa Bahari wa Hormuz unaounganisha Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Oman, na kwamba kuilaumu Iran kwa mashambulizi ya meli za mafuta katika Ghuba ya Oman ni jambo la kushangaza.

Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema kuwa usalama wa dunia nzima, hasa Ghuba ya Uajemi ni muhimu sana kwa Iran hivyo haiwezi kuhusika na chochote katika mashambulizi hayo.

Aidha, Marekani hapo jana iliituhumu Iran kwa mashambulizi ya meli mbili za mafuta katika Ghuba hiyo ya Oman, hatua iliyopelekea kupanda kwa bei za mafuta na kuzua wasiwasi kuhusu mapambano mapya kati ya Marekani na Iran.

Hata hivyo, bado haijulikani ni kitu gani kilichosababisha mlipuko huo uliopelekea mabaharia kuzikimbia meli hizo mbili; Front Altair inayomilikiwa na Norway na Kokuka inayomilikiwa na Japan.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 15, 2019
Video: Vinyozi na Wasusi: Tunatumia ujanja | Elimu ya nini? | Kuna magonjwa | TACIP kuwasajili

Comments

comments