Naibu waziri wa afya nchini Iran, Iraj Harrich ameambukizwa virusi vya Corona, imeelezwa kuwa waziri huyo kwa sasa ametengwa katika eneo maalumu na anaendelea na matibabu chini ya uangalizi.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa naibu waziri huyo amegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo baada ya kuonyesha daliliza homa kali na kufanyiwa vipimo.

Taarifa zinasema kuwa mpaka sasa ugonjwa huo umeua watu 16 nchini humo huku idadi ya maambukizi ikiongezeka kwa kasi.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya nchini humo imesema kuwa ”watu 65 wameambukizwa virusi hivyo mpaka sasa huku idadi ya visa vipya ikiongezeka siku hadi siku”

Hata hivyo Iran ni miongoni mwa nchi ambazo zipo hatarini katika maambukizi ya ugonjwa huo unaosambaa kwa kasi katika nchi mbalimbali duniani.

Balozi Mongela: Ni hasara kuwa na wanawake viongozi wenye aibu
India: Waandamanaji zaidi ya 10 wauawa