Iran imetangaza kifo cha mjumbe wa baraza la kidini linalomchagua kiongozi mkuu wa nchi hiyo, kutokana na virusi vya corona.

Shirika la habari la Iran, IRNA, limearifu kuwa Ayatollah Hashem Bathayi Golpayegani mwenye umri wa miaka 78, amefariki hospitalini alikokuwa amelazwa kwa muda wa siku mbili.

Alikuwa mwakilishi wa jiji la Tehran katika jopo la wataalamu 88 linalomchagua kiongozi wa juu wa Iran na kufuatilia utendajikazi wake.

Takwimu rasmi za serikali ya Iran zinaonyesha kuwa watu takribani 14,000 wameambukizwa virusi vya corona nchini humo, na miongoni mwao 724 tayari wameaga dunia.

Wanasiasa 12 wa ngazi za juu ni miongoni mwa waliouawa na virusi hivyo, na 13 wanao ugonjwa huo na wametengwa katika karantini.

FIGC waomba EURO 2020 iahirishwe
FA washauriwa kufunga ukurasa wa 2019/20