Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema kuwa janga la virusi vya corona limetikisa uchumi wa dunia na litasababisha mdodoro mkubwa wa uchumi wenye athari mbaya kushinda zile za mzozo wa kifedha wa mwaka 2008.

Akizungumza na waandishi habari kwa njia ya video mjini Washington, Mkurugenzi Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amezitaka nchi tajiri kuongeza juhudi za kuyasaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana na athari za janga la corona.

Kiongozi huyo wa IMF amesema kuwa ugonjwa wa COVID-19 umeathiri kwa sehemu kubwa uchumi na uwekezaji katika mataifa yanayoendelea akisema wawekezaji wameondoa mitaji ya hadi dola bilioni 90 kutoka mataifa hayo.

Hayo yanajiri wakati watu zaidi ya milioni moja wakiwa wameambukizwa virusi hatari vya corona duniani huku idadi ya waliokufa ikipanda na kufikia watu zaidi ya elfu sitini.

Wamarekani watakiwa kujiandaa ongezeko vifo vya Corona
Waitara akemea wanopuuza masharti ya kujikinga na Corona