Malaysia imethibitisha kuwa kipande kikubwa cha bati kilichookotwa ufukweni mwezi Juni katika kisiwa cha Pemba, Zanzibar ni cha ndege yake iliyopotea kimaajabu mwaka 2014, MH 370.

Kwa mujibu wa Reuters, Waziri wa uchukuzi wa Malaysia, Liow Tiong Lai amesema kuwa kipande hicho kimethibitika baada ya kukamilika kwa kazi ya uchunguzi iliyofanywa na jopo la wataalam wa Usalama wa Safari za Ndege ya Australia (ATSB) kwa kushirikiana na jopo la wataalam waliokuwa wakichunguza usalama wa ndege ya MH 370.

Sehemu hiyo ya mabaki iliyopatikana Pemba ilikuwa ikionesha muhuri wenye tarehe ya kuundwa kwa ndege hiyo ambayo ni Januari 23, 2002.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitoweka angani mwezi Machi, 2014 ikiwa na abiria 239 ilipokuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea jijini Beijing.

Tiong Lai ameeleza kuwa bado wanaendelea kufanyia utafiti mabaki hayo kutafuta uwezekano wa kupata chanzo cha ndege hiyo kupotea anagani.

Video: Serikali kuwaachia wafungwa chini ya mpango wa Parole
Wizara ya Mambo ya Nje kufanya matembezi kuchangia waathirika tetemeko la ardhi