Sheikh Osman Sharubutu Imamu Mkuu nchini Ghana amesherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuhudhuria misa ya kanisa katoloki.

Kiongoz huyo wa dini mwenye umri wa miaka 100 ni mtu mwenye maneno machache na anauwezo wa kuwaleta watu pamoja akiwa ameketi katikati ya waumini wa Kikristo katika kanisa katoliki la Christ the King Catholic mjini Accra wakati wa ibada ya pasaka imezua gumzo katika mitandao ya kijamii

Mufti huyo mkuu wa Ghana anataka kuhakikisha ameacha utawala wa amani katika uongozi wake ni sehemu ya kuleta jamii pamoja bila kujali misingi yao ya kidini.

Hatua yake ya kuingia kanisani ilishahabiana na kisa cha makanisa kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Kiislam nchini Sri Lanka, ambapo watu zaidi ya 250 waliuawa makanisani na katika Hoteli za kifahari.

Aidha Wale wanaounga mkono hatua ya imam huyo walimtaja kama nuru inayoangaza gizani.

Hata hivyo sio kila mtu aliyefurahishwa na hatua ya Sheikh Osman Sharubutu wengine walisema ni laana, kwa muislamu kushiriki sala ya kikristo.

Lakini Sheikh Sharubutu anasisitiza kuwa hakuwa anashiriki maombi bali hatua yake ilikuwa ya kuimarisha uhusiano kati ya Waislamu na Wakriristo.

“Kiongozi huyu anajaribu kubadilisha dhana potovu kuhusiana na dini ya Kiislamu, kwamba ni dini inayochukia dini zingine,” msemaji wake Aremeyao Shaibu aliiambia BBC.

Spika ahoji serikali kukwama ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
Wanafunzi 8 wapata ujauzito Makete