Jeshi la Polisi nchini limewahakikishia wananchi kuendelea kuwepo kwa hali ya usalama, Amani na kuendelea na hali ya utulivu katika chaguzi ndogo hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara katika Shule ya Polisi Moshi (CCP) ambapo ambapo amezungumza na Wakufunzi na Askari waliopo mafunzoni Chuoni hapo ikiwa na lengo la kukagua mwenendo wa mafunzo yanayoendelea katika Vyuo vya Polisi nchini.

Amesema kuwa katika maeneo yaliyofanya uchaguzi mdogo hali ilikuwa shwari licha ya kuwepo kwa matukio madogo ambayo yanaendelea kushungulikiwa na upelelezi utakapokamilika majalada yao yatapelekwa kwa Waendesha mashtaka kwa hatua zaidi.

“Hali iliuwa shwari na ni wazi kuwa wananchi sasa wameelewa umuhimu wa kutii sheria bila ya kushurutishwa na natoa rai waendelee kudumisha hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za Wahalifu.” amesema

 

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Mungi amesema kwa Chuo hicho kinaendelea kutoa mafunzo kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa kila Askari anayetoka anakuwa na ukakamavu wa kutosha na nidhamu ya kuwahudumia Wananchi.

Mfumo wa Maurizio Sarri wamkimbiza Bakayoko
Fanyeni kazi acheni 'Kiki'- Jafo