Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewataka askari wa Jeshi hilo kote nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa, utovu wa nidhamu na badala yake kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Ameyasema hayo akiwa mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ambapo amesema kuwa, Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameendelea kuufanya mkoa huo kuwa katika hali ya usalama.

IGP Sirro akiwa mkoani Mara, amefanya ukaguzi wa mradi wa nyumba za makazi ya askari ambapo hadi kufikia sasa maendeleo ya mradi huo yamefikia hatua ya kukamilika kwa nchi nzima huku Rais Dkt. John Magufuli akitarajiwa kuzindua nyumba 114 zilizojengwa huku matarajio ya ujenzi huo ni kuwa na jumla ya nyumba 400 nchi nzima.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 13, 2019
Jafo atoa neno kuhusu shule za serikali, 'Msihangaike kuwahamisha watoto'