Idadi ya waliofariki kutokana na msongamano wa watu katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mjini Morogoro imeongezeka na kufikia wawili baada ya mtu mmoja kufariki siku moja baada ya rais Jakaya Kikwete kuwatembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa ya Morogoro.

Mwanachama huyo wa CCM aliyefariki hospitalini hapo alitajwa kwa jina la Grace Geoge mkazi wa Kilakala. Grace aliyekuwa na umri wa miaka 46, alifariki wakati akikimbizwa hospitali kutokana na kuwa na hali mbaya.

Taarifa zinaelezwa kuwa maafa hayo yalitokea baada ya sintofahamu iliyozuka karibu na geti la kutokea na kupelekea watu waliokuwa wamesongamana kukanyagana. Tukokana na tukio hilo, watu zaidi ya 19 wameripotiwa kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro. Mganga mkuu wa hospitali hiyo alithibitisha kupokea idadi hiyo ya majeruhi pamoja na watu wawili waliopoteza maisha.

Rais Jakaya Kikwete ambaye alihudhuria mkutano huo, aliwatembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa ya Morogoro na kuwapa pole walioathiriwa na tatizo hilo.

Rais Kikwete pia alishauri uwanja huo kufanyiwa ukarabati wa milango na kuhakikisha kuwa wakati wa mikutano mikubwa kama hayo milango yote inafunguliwa ili tukio kama hilo lisitokee tena.

Pizarro Arejea Werder Bremen
Ahadi Mpya Ya Ukawa, Lowassa Na ‘Kaunt Daun’ Yake