Wizara ya afya Tanzania  imetoa taarifa leo Machi 30,2020 imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa Covid 19 baadaya kufanyiwa vipimo katika maabara kuu ya Taifa.

Taarifa hiyo imesema kuwa kati ya wagonjwa hao watatu (3) ni kutoka Dar es salaam na wawili(2) kutoka Zanzibar ambapo taarifa zao zilitolewa na waziri wa afya Zanzibar.

Ambapo mpaka hivi wagonjwa wa Covid 19 nchini ni kumina tisa (19) akiwemo mgonjwa mmoja aliyetolewa taarifa na waziri wa afya Zanzibar machi 23,2020.

Aidha wagonjwa wapya Dar es Salaam ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49 mtanzania alikutaana na raia wa kigeni kutoka katika nchi zilizoathirika zaidi, mwanamke mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wanafuatiliwa, na mwanaume miaka 49 ambaye pia ni miongoni mwa watu waliokuwa wanafuatiliwa.

Hata hivyo kazi ya kufuatilia watu wote wa karibu waliokutana na wagonjwa hao inaendelea.

Mshtuko: afariki maduka yake mawili yakiteketea moto
Canada: Mke wa waziri Mkuu apona Corona

Comments

comments