Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amewataka mashabiki wa timu hiyo kuacha kuimba wimbo unaomkashifu.

Mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakiimba wimbo unaomtaja Lukaku huku pia wakitaja jinsi maungo ya siri ya mwanasoka huyo yalivyo jambo ambalo limetafsiriwa vibaya na watu wengi japo mashabiki hao wanaliimba kwa sifa.

Wimbo huo umekuwa maarufu sana katika siku za usoni ambapo mwanzo ulikuwa unaimbwa na kikundi kidogo tu cha mashabiki lakini baadae wimbo huo umezagaa kwa mashabiki wengi wa Manchester United.

Tayari chama cha soka nchini Uingereza FA kimekwishaionya Manchester United kuhusu wimbo huu na kuitaka klabu hiyo kutafuta namna kuona ni kwa jinsi gani wanaweza wakawazuia mashabiki kuimba wimbo huo.

Sikiliza wimbo huo unaoibwa na mashabiki wa Man Utd hapa chini,

Romelu Lukaku naye anaonekana kuchoka na sasa anaomba heshima itawale kati yake na mashabiki “ni faraja ninavyoungwa mkono na mashabiki wa Manchester United na nyimbo zao lakini tuheshimiane” aliandika Lukaku.

Kiongozi wa Korea Kaskazini ajibu vitisho vya Trump, ‘itamgharimu’
Wenye vyeti feki kurejesha mishahara waliyolipwa