Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imependekeza mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kusimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia tarehe ya azimio.

Hatma hiyo ni kufuatia Mbunge huyo kuunga mkono hoja iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali CAG, Mussa Assad kuwa Bunge ni dhaifu.

Ambapo jana Spika wa Bunge Job Ndugai aliagiza kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji Lema ili athibitishe kama kweli Bunge ni dhaifu.

Adhabu hiyo inaendana na ile iliyotolewa kwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee, ambaye nae kwa upande wake aliunga mkono hoja ya kudai kuwa Bunge ni dhaifu ambapo yeye ametakiwa kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge.

Aidha Spika Job Ndugai amesema kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio dhaifu kama ambavyo wachache wamekuwa wakisema na yupo tayari kuthibitisha kuwa Bunge lina uongozi Imara na kuwa hakuna mtu yeyote anayeogopwa.

”Wanaofikiri sisi dhaifu, sio dhaifu. Yeyote ambaye anataka kuingia kwenye 18, tupo tayari, tunataka kuthibitisha Bunge lina uongozi, hatumuogopi yeyoye” Amesema Spika Job Ndugai.

Video: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi kituo cha afya cha Mbonde, Masasi - Mtwara
Video: CAG wingu zito, Msekwa alishangaa bunge