Hukumu katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya wafanyabiashara watatu akiwemo raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama Malkia wa Tembo, inatarajiwa kutolewa Februari 19, katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu.

Glan na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya jinai ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya sh bilioni 13 kinyume cha sheria.

Kesi hiyo ilitakiwa kutolewa hukumu jana na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya kisutu, Huruma Shaidi, lakini aliahirisha ili kumalizia baadhi ya vitu vinavyohusisha hukumu ya kesi hiyo.

Mbali na malikia wa tembo washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase, ambao wote wanatetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Hassan Kaigo.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mahakamani hapo mashahidi 11 kwa ajili ya kuthibitisha mashtka yao na baadae mahakama ikawakuta na kesi ya kujibu washtakiwa hao.

Mawakili watetezi wa washtakiwa walipotakiwa kujitetea waliwasilisha maelezo yao ya kuomba mahakama iwaachie huru.

Ikumbukwe kuwa washtakiwa wa kesi hii wanadaiwa kuwa mnamo Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali.

Video: Makonda amjibu Tundu Lissu, Simba hii sasa sifa
Baada ya kipigo kutoka kwa Simba, Yanga yasubiri adhabu kutoka TFF

Comments

comments