Mara baada ya rappa Meek Mill kuilalamikia hoteli ya Cosmopolitan iliyopo mjini Las Vegas nchini Marekani  kwa ubaguzi wa rangi imeripotiwa kuwa hoteli hiyo imepanga kuomba radhi hadharani kwa kitendo hicho ambacho kilitokea Jumapili ya May 26.

Hata hivyo mwanasheria wa msanii huyo Joe Tacopina alitoa taarifa kuwa atafungua shauri wiki hii dhidi ya hoteli hiyo kwa kumzuia Meek Mill kuingia katika hoteli hiyo kwaajili ya kuhudhuria tamasha la Dj Mustard

Hata hivyo walinzi wa hoteli hiyo walisema kuwa Meek Mill alizuiliwa kutokana na sababu walizozitaja kuwa hakufuata utaratibu wa kuingia hivyo watamkamata.

Aidha Meek Mill aliposti  video mtandao wa kijamii Instagram akidai kuwa ubaguzi wa rangi umetawala.

Iliripotiwa kuwa Mwanasheria wa rapper huyo, Joe Tacopina aliandika barua ikiwataka wamiliki wa hotel hiyo kuomba radhi kwa kitendo hicho ikiwa ilielezwa kuwa ni tabia ya hoteli hiyo kuwazuzia mastaa weusi kuingia mahali hapo.

 

 

Video: Ufahamu ugonjwa wa Ini hatari zaidi ya Ukimwi, hauna tiba, dalili, maambukizi
Bangi yamponza, asukumwa ndani miaka 30

Comments

comments