Takribani wafungwa 1,350 wametoroka katika gereza lililoko Pwani ya São Paul nchini Brazil wakihofia kuambukizwa virusi vya corona (Covid-19).

Imeelezwa kuwa vuguvugu la kugoma na kutoroka lilianza baada ya zuio la wafungwa hao kuondolewa kwa muda gerezani wakati wa msimu ujao wa Pasaka, uamuzi uliochukuliwa na uongozi wa gereza ili kuepuka wafungwa wanaorudi gerezani kuwa na hatari ya kubeba maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19).

Hata hivyo, ilizuka taharuki iliyotokana na taarifa za kuwepo kwa baadhi ya walinzi wa gereza hilo ambao wameathirika na virusi vya corona, taarifa ambazo hazikuwa zimethibitishwa. Imeelezwa kuwa wafungwa hao waliwateka baadhi ya askari ili kufanikisha lengo lao la kutoroka.

Kwa mujibu wa ‘The Sun’, Jeshi la Polisi la Brazil lilifanikiwa kuwakamata wafungwa 41 na kuwarudisha gerezani.

Askari tisa waliokuwa wameshikiliwa mateka na wafungwa wameachiwa na wafungwa ambao hawakuwa wametoroka walirejea kwenye selo zao, kwa mujibu wa taarifa hizo.

 


Serikali ya nchi hiyo ilichukua hatua za tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzuia watu wa nje kuwatembelea wafungwa hao kwa muda.

Jumatatu, Machi 16, 2020 Mahakama ilisitisha kusikiliza kesi kwa mkusanyiko kama tahadhari dhidi ya virusi vya corona.

Tanzania, Ubelgiji zajadili kuboresha sekta ya kilimo na Madini… Sweden yaahidi ushirikiano
Tahadhari ya Corona, CCM yasitisha mikutano ya ndani na hadhara